1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghasia za Msumbiji kutawala mkutano wa kilele wa SADC

Sylvia Mwehozi
16 Novemba 2024

Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC wanakutana kuanzia leo katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare, kuujadili mzozo wa Msumbiji.

Mkutano wa SADC  mjini Harare mwezi Agosti 2024
Mkutano wa viongozi wa SADC Agosti -2024Picha: Tafara Mugwara/Xinhua/IMAGO

Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC wanakutana kuanzia leo katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare, kuujadili mzozo wa Msumbiji.

Mzozo wa kisiasa na kijamii unaozidi kuongezeka Msumbiji utakuwa ndio ajenda kuu ya mkutano wa kilele wa SADC ulioitishwa baada ya matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 9 kusababisha maandamano ya wiki kadhaa na kumfanya mgombea wa upinzani aliyeshindwa kupinga matokeo.

Watu wasiopungua 30 wanaripotiwa kuuawa katika maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi kufuatia ushindi wa mgombea wa chama tawala cha FRELIMO Daniel Chapo.

Kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane anayapinga matokeo hayo ambayo anadai kuwa yamechakachuliwa na kuitisha maandamano ya nchi nzima.

Miito imekuwa ikitolewa ili kurejeshwa hali ya utulivu na utawala wa sheria nchini Msumbiji.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW