Mzozo wa Kisiwa cha Migingo
13 Mei 2009Matangazo
Tamko la karibuni la Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ni kwamba kisiwa hicho ni cha Kenya, lakini maji yanayozunguka kisiwa hicho ni ya Uganda. Kuna wabunge huko Kenya, hasa kutoka eneo la Nyanza, wanaotaka kuwahimiza wananchi wachukue hatua ya kukimiliki kisiwa hicho, ikiwa mkuu huyo wa Uganda atasita sita kuhusu jambo hilo.
Othman Miraji alizungumza kwa njia ya simu na waziri wa nchi katika wizara ya mambo ya kigeni ya Uganda, Okello Oryem, kutaka ufafanuzi kutoka kwake kuhusu matamshi ya Rais Museveni:
Mwandishi: Othman Miraji
Mhariri: Mohamed Abdulrahman