1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mzozo wa Kosovo na Serbia wazidi kushika makali

15 Juni 2023

Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti, ameamuru kuimarishwa kwa ulinzi kwenye mpaka na nchi jirani ya Serbia kufuatia madai aliyoyatoa kwamba Serbia imewateka nyara maafisa watatu wa polisi ya Kosovo.

Spannungen im Kosovo
Picha: MICHAL CIZEK/AFP/Getty Images

Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti, ameamuru kuimarishwa kwa ulinzi kwenye mpaka na nchi jirani ya Serbia

Akizungumza na waandishi habari kwenye mji mkuu Pristina, Kurti amesema ukaguzi wa mpakani utaimarishwa na idadi ya magari yanayotoka Serbia itapunguzwa.

Kulingana na waziri Mkuu Kurti, Serbia ndiyo inabeba dhima ya hali hiyo kutokana na kitendo chake cha kuwakamata walinzi watatu wa mpakani ndani ya ardhi ya Kosovo.

Serbia imeyapinga vikali madai hayo kupitia kwa rais wake Aleksandar Vucic aliyesema maafisa hao walikamatwa ndani ya ardhi ya Serbia wakiwa wamebeba bunduki za rashasha.

Kisa hicho ni mwendelezo wa mvutano unaozidi makali kati ya Serbia na Kosovo iliyowahi kuwa sehemu ya Serbia kabla ya kujitangazia uhuru mwaka 2008.

Pande hizo mbili zimo kwenye mzozo wa muda mrefu unaochochewa na uamuzi wa Serbia wa kutoutambua uhuru wa Kosovo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW