1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa Ugiriki watikisa masoko

4 Oktoba 2011

Hisa duniani zilianguka hapo jana na sarafu ya euro ilishuka kwa kiwango kilicho chini katika muda wa miezi 8 na nusu dhidi ya dola kutokana na kuzidi wasiwasi kuwa inawezekana Ugiriki itashindwa kulipa madeni yake

Nembo ya Euro

Mawaziri wa fedha wa nchi 17 zinazoitumia sarafu ya euro wamekutana mjini Luxembourg kujadili hali iliopo wakati huo huo wakaguzi wa kutoka Umoja wa Ulaya na shirika la fedha la kimataifa, IMF, na benki kuu ya Ulaya, walifika nchini Ugiriki kuona iwapo nchi hiyo inafaa kupokea awamu nyengine ya mkopo wenye thamani ya euro bilioni 8, ya mkopo wake wa euro bilioni 110.

Picha: dapd

Siku ya Jumapili Ugiriki ilikiri kuwa huenda ikakosa kufikia kupunguza nakisi yake ya asilimia 7.7 katika bajeti yake mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya masharti iliyopewa ili kupokea mkopo huo mpya.

Waziri wa Fedha wa Ugiriki Evangelos VenizelosPicha: dapd

Katika rasimu ya bajeti iliyotolewa bungeni hapo jana bunge la nchi hiyo ilitabiri nakisi ya asilimia 8 na nusu ya pato lake jumla kwa mwaka huu, 2011.

Mwandishi Maryam Abdalla/AP, dpa

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW