Mzozo wa Uturuki na mataifa ya Ulaya
15 Machi 2017Mhariri anasema kwamba Chaguo bado lingali wazi, kwa sababu wengi miongoni mwa Waholanzi bado hawajaamua. Kitu kimoja kingali wazi nacho ni kwamba vyama vinavyounda serikali ya mseto vitapoteza kura. Lakini pamoja na hayo vyama hivyo vitahakikisha chama cha siasa kali za kizalendo za mrengo wa kulia kinashindwa. Sababu ni kwamba Rais Erdogan wa Uturuki ni mfano mmoja mzuri wa kile kinachoweza kutokea pindi wenye siasa kali za kizalendo wanaingia madarakani.
Gazeti la Westfälische Nachrichten: Mhariri ameandika hivi,Nani anayetaka vitisho, matusi na kufananishwa na Wanazi na wakati huo huo ajadiliane na Uturuki ? Huu sio tu ni mzozo wa kidiplomasia, lakini huenda Uturuki ikajikuta ikitengwa kisiasa kwa muda mrefu. Mazungumzo na Umoja wa Ulaya kwa wakati huu hayana tija.
Kujiondoa kwenye mihimili ya kidemokrasi na ukiukaji wa Haki za binaadamu, kunaifungia njia Uturuki ya kuelekea Ulaya ilio huru na yenye amani."
Hannoversche Allgemeine Zeitung llimeandika juu ya mabishano kati ya Scotland na serikali kuu ya Uingereza inayoongozwa na Theresa May kuhusu mpango wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya:
Uingereza inatarajiwa kuanza mchakato wa kujitoa rasmi katika Umoja wa Ulaya. Jee Uhuru wa Scotland inayopinga mpango huo ndiyo Suluhisho. Huenda kukawa na nafasi chungu nzima pindi hilo likitokea, lakini pia kuna athari nyingi mpya . Kutokana na hayo wanaopinga Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya wamekuwa wakati wote wakionya kwamba Itakuwa zawadi kubwa kwa Waingereza kusema Kwaheri Umoja wa ulaya , kwani kwa huenda ikwa ni tija kwa Scotland- tija ya kutaka kujitenga.
Neue Osnabrücker Zeitung limezingatia uamuzi wa Mahakama kuu ya Ulaya kwamba waajiri wanaweza kupiga marufuku uvaaji wa vazi la hijabu makazini:
Uamuzi wa mahakama kuu ya Ulaya ni wakusisimua kwa sababu ni kuhusu haki za msingi. Dini ni jambo la binafsi na hata waajiri wamelazimika kukubaliana nalo. Kuna tafauti kati ya uhuru wa kuabudu na haki za kibiashara. Uamuzi huo wa mahakama kuu ya Ulaya unafafanua kwamba uhuru wa kuabudu katika jamii ya mchanganyiko wa watu wa dini tafauti hauna mipaka. Sasa ni juu ya mwajiri mwenyewe kuamua ,anapiga marufuku au la. Na hiyo ni ishara kamili ya kuwepo kwa uhuru na kuvumiliana.."
Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman/ Dt Zeitungen
Mhariri:Yusuf Saumu