1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa Zimbabwe unatiwa chunvi,inasema jumuia ya SADC

18 Agosti 2007

Lusaka:

Jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC inahisi matatizo ya Zimbabwe yametiwa chunvi”amesema hayo mwenyekiti mpya wa jumuia hiyo,rais Levy Mwanawasa,mwishoni mwa mkutano wa SADC jana usiku mjini Lusaka.”Tumeridhika na sheria ya upigaji kura nchini Zimbabwe,inayoruhusu uchaguzi huru na wa haki” amesema kiongozi huyo wa Zambia wakati wa mkutano pamoja na waandishi habari mjini Lusaka.Tangu miaka minane iliyopita,Zimbabwe imekua ikizidi kutumbukia katika janga la ughali uliokithiri wa maisha-kuporomoka kiwango cha bidhaa zinazolimwa nchini humo na kuzidi kiwango cha watu wasiokua na ajira kinachofikia asili mia 80.Mashahidi wanazungumzia pia juu ya kuvunjwa haki za binaadam.Jumuia ya kimataifa inawashinikiza viongozi wa jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika wasake ufumbuzi wa mzozo wa Zimbabwe..Viongozi wa jumuia hiyo ya SADC lakini wanaonyesha wanamvumilia zaidi rais Robert Mugabe,mzee wa miaka 83-anaesifiwa kua shujaa wa mapambano dhidi ya ukoloni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW