Mzozo wa Zimbabwe
5 Desemba 2008
Rais Robert Mugabe amesema ataitisha uchaguzi wa mapema iwapo makubaliano ya kugawana madaraka na upinzani hayatafanikiwa katika muda wa miaka miwili ijayo. Kwa upande mwingine Marekani imetoa msaada wa dolla elfu 600 kwa zimbabwe ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu ambao umesasabisha vifo ya mamia ya wazimbabwe katika muda wa wiki chache zilizopita.
Hatua ya marekani kutoa msaada huo wa kifedha, imetokana na ombi la zimbabwe la kutaka msaada wa kimataifa baada ya kutangaza ugonjwa wa kipindu pindu ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 560 kuwa janga la kitaifa.
Katika taarifa shirika la misaada ya maendeleo la marekani USAID, limesema pesa hizo zitatumika katika kukabiliana na kuzuka kwa ugonjwa huo.
Msaada huo na shirika hilo, unafikisha kiasi cha fedha zilizotolewa na marekani kwa zimbabwe kutokana na uhaba wa chakula na pia kuisadia secta yake ya afya kuwa zaidi ya dolla millioni 220 tangu october mwaka jana..
Naibu msemaji wa wizara ya nje ya marekani Robert Wood aliwaambia wanahabari kuwa marekani inafwatilia kwa makini matukio nchini zimbabwe kuanzia secta ya afya, kiuchumi na hata hali ya kisiasa.
Kwa mara nyingine aliitaka serikali ya rais Mugabe kutekeleza makubaliano ya kugawana madaraka na upinzani. Akinukuliwa na gazeti linalomilikiwa na serikali la The Herald rais Mugabe naye amesema iwapo makubaliano hayo hayatafanikiwa katika muda wa miaka miwili ijayo basi itabidi kufanywa kwa uchaguzi mkuu wa mapema. Rais mugabe alisema na namnukuu…“tulikubaliana kuupa upinzani wizara 13 huku tukigawana wizara ya mambo ya ndani. lakini iwapo makubaliano hayo yatafeli katika muda wa mwaka mmoja unusu au miaka miwili ,basi itatubidi kufanya tena uchaguzi',mwisho wa nukuu.
Serikali ya rais Mugabe imekabiliwa na panda shuka nyingi tangu alipopoteza katika raudi ya kwanza ya uchaguzi mkuu wa mwezi marchi, na kisha baadaye kujitangaza mshindi katika raundi ya mwisho ya uchaguzi huo uliosusiwa na na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.
Hali mbaya ya miundo msingi imesadia kufanikiwa kuenea kwa haraka kwa ugonjwa wa kipundupindu huku zaidi za visa elfu 12 vikiripotiwa.
Uingereza nayo imetangaza kutoa msaada wa dolla millioni 14.7 kwa Zimbabwe.Waziri mkuu wa uingereza Gordon Brown alimshutumu rais Mugabe kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali nchini zimbabwe.Waziri mkuu wa kenya Raila Odinga naye amezitaka serikali za afrika,kuchukua hatua zitakazomuondoa madarakani rais Robert Mugabe.
Matamshi hayo ya Raila yanawadia baada ya kufanya mashauri na kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai ambaye amekuwa akizuru mataifa mbalimbali ya bara uropa na afrika katika haraka za kutaka kuungwa mkono.
Rais Mugabe na Tsvangirai walitia saini makubaliano ya kugawana madaraka zaidi ya miezi mwili iliyopita,lakini wamekosa kukubaliana njisi ya kubuni serikali ya umoja wa kitaifa.
Askofu mkuu wa afrika kusini Desmond Tutu pia yumo katika orodha ya wale wanaotaka rais Mugabe kuondolewa kwa lazima madarakani.
Wakati huo huo afrika kusini wiki ijayo itawatuma viongozi wake wakuu serikalini nchini Zimbabwe ili kutathimi hali ya chakula ilivyo.