1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozozo wa Fedha-Marekani

Eric Kalume Ponda12 Desemba 2008

Mgogoro wa sekta ya fedha nchini Marekani unaendelea kutikisa uchumi wa Marekani, huku sekta ya viwanda vya magari ikikabiliwa na tisho la kuporomoka.

Kampuni ya magari ya General Motors na Chrysler nchini Marekani zakumbwa na tisho la kuporomoka.Picha: picture-alliance/dpa


Hii ni baada ya bunge la Senate kushindwa kuafikiana kuhusu mpango wa kuikoa sekta hiyo kufuatia hali ngumu ya kiuchumi.


Bunge hilo lilitarajiwa kujadiliana kuhusu mpango wa dola bilioni 14 uliopendekezwa na chama cha Demokrat katika juhudi za kuikoa sekta hiyo.Hatua hiyo hiyo sasa imetoa ishara ya hali ngumu na kutikisa soko la sekta ya magari katika eneo zima la Asia.



Mpango huo ulikusudiwa kuzipa mikopo na kuziokoa kampuni kubwa za magari nchini Marekani,ikiwa ni ile ya General Motors na Chrysler ambazo zinakumbwa na tisho la kuporomoka, ili kuweziwezesha kufadhili shughuli zao hadi Machi 31 mwaka ujao,kufuatia mgogoro huo wa kiuchumi.


Kampuni hizo mbili zilitoa onyo kwamba huenda zikaporomoka iwapo hazitaokolewa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi inayoyakumba, na hivyo kupelekea kuachishwa kazi kwa zaidi ya wafanyi kazi 250,000, na wengine 100,000 wanaotegemea kampuni hizo.


Mapngo huo wa dola bilioni 14 uliopitishwa na bunge la waakilishi wiki iliyopita, umekabiliwa na upinzani mali hasa kutoka kwa wabunge wa chama cha Republican wakati ulipokuwa ukijadiliwa bungeni.


Badala yake wabunge wa chama hicho cha Republican walipendekeza nyongeza ya viwango vya misharaha ya wafanyi kazi wa viwanda vya magari nchini Marekani kuanzia mwaka ujao ili kuviambatanisha na vile vinavyolipwa wafanyi kazi katika viwanda vya nmataifa ya kigeni.


Wabunge hao wa Republican walisema kuwa iwapo bunge hilo litapitisha mpango huo, hiyo itakuwa sawa na kuiweka sekta hiyo chini ya usimamizi wa serikali.


Mgogoro huo wa kiuchumi umepelekea watu wengi nchini Marekani kuendelea kuachishwa kazi ,huku Rais George W Bush na Rais mteule Barrak Obama,wote walikubaliana kwa kauli moja kwamba hali hiyo haiwezi kuachwa kuendelea zaidi.


Huku bunge hilo likijadilia suala hilo, zaidi ya wafanyi kazi 35,000 katika benki ya Marekani, wameachishwa kazi, hali inayoelezea dhahiri jinsi mgogoro huo wa kiuchumi unavyoendelea kuathiri sekta ya fedha nchini humo. Hii inafuatia kuachishwa kazi kwa zaidi ya wafanyi kazi 50,000 wa benki ya Citigroup mwezi uliopita.


Tayari hatua iliyochukuliwa na bunge hilo ka Senate imetikisha soko la magari katika mataifa ya Asia, ambapo viwango vya mauzo vilishuka kwa jumla ya kati ya asilimia 3 na 5.


Kwa mfano viwango vya mauzo katika kampuni ya magari ya Toyota vilishuka kwa asilimia 10, Honda vikashuka kwa asilimia 13, Nissan ikapoteza asimilia 12 kufuatia kushuka kwa hisa nchini Japan.


Wakati huo huo viongozi wa mataifa ya Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Brussel,wanatarajiwa kuanza awamu ya pili ya mazungumzo kuhusu mpango wa Euro billioni 200, sawa na kiwango cha dolla bilioni 260 kuokoa sekta ya fedha katika eneo lao.


Kwa upande wake Japan ambayo uchumi wake umetikisika zaidi kufuatia hatua ya iliyoafikiwa na bunge la Marekani, imetangaza hatua madhubuti za kuokoa uchumi wake.


Serikali hiyo inasema kuwa itatenga kiasi cha dola bilioni 437 kuokoa sekta ya kiuchumi nchinim mwaka baada ya zaidi ya watu 380 kupoteza kazi nchini humo.



Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW