Nachafuko katika bunge la Georgia
22 Novemba 2003Matangazo
TIFLIS: Nchini Georgia wafuasi wa upinzani wamelivamia bunge na kumlazimisha Rais Edward Shewardnadse akimbie kutoka jengo hilo la bunge. Rais Shewardnadse, mwenye miaka 75, alichukuliwa na kutolewa bungeni na walinzi wake alipokuwa akikihutubia kikao cha mafunguzi cha bunge lililochaguliwa hivi karibuni tu. Muda si muda yalitokea mapigano kati ya wafuasi wake na wavamizi. Baada ya hapo kiongozi wa upinzani Michali Saakashvill alizungumza bungeni juu kile alichokiita "Harakati za Mapinduzi Baridi Nchini Georgia". Kabla ya hapo watu waliandamana kwa maelfu katika njia za mji mkuu Tiflis na kumwita ajiuzulu Rais Shewardnadse. Kwanza wanajeshi na polisi walizingira barabara na kuwazuiya wasingie bungeni wafanya machafuko hao, lakini hatimaye walishindwa nguvu. Chanzo cha machafuko hayo kinatokana na uchaguzi wa bunge uliofanyika wiki chache zilizopita. Ripoti za vyombo vya habari ziliwafikiana kwamba kilifanyika kiini macho cha kura katika uchaguzi huo.
