1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nagelsmann abadili kikosi Ujerumani dhidi ya Ghana

30 Machi 2026

Alexander Nübel ndiye atakayeanza kama mlinda lango wa Ujerumani katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ghana Jumatatu.

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Julian Nagelsmann katika mechi dhidi ya Uswisi
Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Julian Nagelsmann katika mechi dhidi ya UswisiPicha: Christian Charisius/dpa/picture alliance

Haya ni kwa mujibu wa kocha mkuu wa UjerumaniAlexander Nübel anayedai kuwa Oliver Baumann anasalia kuwa kipa nambari moja.

Nübel atakuwa anaichezea Ujerumani kwa mara ya tatu Jumatatu na mchezaji mwenzake katika klabu ya VfB Stuttgart Denis Undav atacheza pia ila haijawekwa wazi iwapo ataanza kwenye kikosi cha kwanza au atakuwa mchezaji wa akiba.

Oliver Baumann anayeichezea klabu ya Hoffenheim alishiriki mechi zote sita za kuwania kufuzu kwenye Kombe la Dunia kipindi kilichopita cha mapukutiko na alikuwa mchumani pia kwenye mechi ya Ijumaa ambapo Ujerumani ilishinda 4-3 dhidi ya Uswisi.

Mabadiliko ambayo kocha Nagelsmann amesema anapanga kuyafanya katika mechi dhidi ya Ghana, huenda yakawaathiri nahodha Joshua Kimmich, mchezaji mwenzake wa Bayern Munich Serge Gnabry na Kai havertz ambaye ndiye mwanzo amerudi kutoka kwenye jeraha la muda mrefu.

Nathaniel Brown wa Eintracht Frankfurt ataanza kama beki wa shoto badala ya David Raum wa RB Leipzig ila Nagelsmann amesema Brown hatocheza kwa dakika tisini.

Hii mechi dhidi ya Ghana ndiyo ya mwisho kwa Ujerumani kabla Nagelsmann kutangaza kikosi chake cha mwisho cha Kombe la Dunia mnamo Mei 12.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW