1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kocha Nagelsmann ataka kujiepusha na "hisia zilizopitiliza"

26 Machi 2024

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Julian Nagelsmann amesema anataka kuepukana na "hisia zilizopitiliza" kufuatia ushindi wa kuridhisha wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Ufaransa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Julian Nagelsmann
Kocha Nagelsmann aliiongoza timu ya taifa kuifunga Ufaransa mabao 2 - 0 katika mechi ya kirafikiPicha: BEAUTIFUL SPORTS/Wunderl/IMAGO

 Akizungumza kabla ya mechi ya kirafiki ya Jumanne usiku dhidi ya Uholanzi, Nagelsmann amesema katika kandanda, lazima uwe na muendelezo mzuri wa matokeo na sio tu kushinda mechi moja na kuhisi kuwa uko katika hali nzuri.

Soma pia: Nagelsmann ashinda mechi ya kwanza na timu ya taifa

Matokeo hayo dhidi ya Ufaransa, mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka wa 2018, yamewafanya mashabiki wa Ujerumani kuwa na msisimko tena wakati wenyeji hao wa mashindano ya Euro 2024 wakikamilisha maandalizi yao ya mwisho kabla ya kinyang'anyiro hicho kuanza katika majira ya joto.

Baada ya vichapo sita na sare mbili katika mechi 11 mnamo mwaka wa 2013, matarajio ya nafasi za timu hiyo mwenyeji wa mashindano ya Ulaya yako chini. Nagelsmann ameongoza mechi tano tangu alipochukua usukani Septemba mwaka wa 2023, ikiwemo vichapo dhidi ya Uturuki nyumbni na ugenini Austria. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 36, amesema anatarajia kuanza mechi dhidi ya Uholanzi na kikosi kile kile kilichoanza dhidi ya Ufaransa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW