1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Nagorno-Karabakh yamchagua rais mpya

9 Septemba 2023

Mkoa wenye idadi kubwa ya Waarmenia wa Nagorno-Karabakh nchini Azerbaijan umemchagua rais mpya huku mvutano kuhusu eneo hilo ukiongezeka kati ya mahasimu wakuu Azerbaijan na Armenia.

Waarmenia wa Nagorno Karabakh waandamana mnamo Julai 25 2023, kupinga kufungwa kwa barabara ya Lachin
Waarmenia wa Nagorno Karabakh waandamanaPicha: Alexander Patrin/TASS/dpa/picture alliance/dpa

Kwa kura 22 dhidi ya moja, wabunge katika bunge la Nagorno-Karabakh wamemchagua mkuu wa baraza la usalama katika serikali hiyo ya uasi, Samvel Shahramanyan, mwenyemiaka 45, kumrithi kiongozi anayeondoka Arayik Harutyunyan aliyejiuzulu mnamo Septemba 1. Azerbaijan imeutaja uchaguzi huo kuwa hatua nyingine ya uchokozi mkubwa na ukiukaji wa wazi wa uhuru wake na uadilifu wa eneo hilo.

Umoja wa Ulaya wasema hautambui mfumo uliotumika kuandaa uchaguzi huo

Umoja wa Ulaya umesema hautambui mfumo wa kikatiba na kisheria uliotumika kuandaa uchaguzi huo, lakini umetoa wito kwa raia wa Armenia walioko katika eneo hilo la Nagorno Karabakh kuungana katika uongozi wa kweli unaoweza na ulio tayari kushiriki katika mazungumzo ya tija na Azerbaijan.