Naibu Kansela wa Ujerumani ahimiza ushirikiano na Ukraine
3 Aprili 2023Ametowa mwito huo baada ya kutembelea kituo kidogo kinachosambaza umeme katika maeneo yanayokaliwa na wakaazi wengi wa Ukraine, kinachoendeshwa na kampuni inayomilikiwa na serikali ya Ukrenergro.
Habeck ameandamana na ujumbe wa wafanyabiashara wa Ujerumani katika ziara hiyo nchini Ukraine. Ujerumani na nchi hiyo zimekuwa na ushirikiano rasmi katika sekta ya nishati tangu mwaka 2020 unaolenga kuimarisha ufanisi wa upatikanaji nishati, kuiboresha sekta hiyo kuwa ya kisasa ,kutanuwa uzalishaji wa nishati jadidifu pamoja na kupunguza uzalishaji wa hewa chafu.
Kiongozi huyo wa Ujerumani amesema kufanikisha malengo hayo ni hatua inayoweza kuifanya sekta ya nishati ya Ukraine kuwa imara zaidi na pia kuigeuza nchi hiyo kuwa msafirishaji mkubwa wa nishati barani Ulaya.