Naibu Kansela wa Ujerumani ziarani Ukraine
3 Aprili 2023Matangazo
Kwa mujibu wa gazeti la the Spiegel la Ujerumani, Habeck ambaye pia ni waziri wa nishati na uchumi atajadili kuhusu suala la ujenzi mpya wa Ukraine pamoja na ushirikiano katika sekta ya nishati.
Ziara ya Habeck imethibitishwa pia na msemaji wa wizara yake ingawa hakutowa maelezo zaidi kutokana na tahadhari za kiusalama.
Sekta ya nishati ya Ukraine imeshambuliwa mara kadhaa na Urusi katika vita vinavyoendelea na baadhi ya wakati mamilioni ya watu waliachwa kizani kutokana na kuharibiwa kwa miundo mbinu ya umeme.