1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Jan Egeland anapigania uitishwe mkutano wa wafadhili wa kimataifa kwaajili ya maziwa makuu

3 Septemba 2005

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Jan Egeland amelalamika walimwengu hawatilii maanani hali namna ilivyo katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo..Bwana Jan Egeland amesema nchi hiyo ya maziwa makuu inakumbwa na balaa kubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa ulimwenguni.Amelinganisha maafa yanayowafika wakaazi wa Kongo Kinshasa na yale ya wakaazi wa maeneo yaliyokumbwa na Tsunami kusini mashariki ya Asia.Akihojiwa na gazeti la Ubiligiji „Le Soir“ naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Jan Egeland amelalamika akisema ulimwengu hautilii maanani kipeo cha balaa linalotokea jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo,Burundi na Rwanda.Bwana Egeland alikua mjini Brussels ambako alionana na kamishna wa Umoja wa Ulaya anaeshughulikia masuala ya maendeleo bwana Louis Michel na waziri wa misaada ya maendeleo wa Ubiligiji Armand De Decker.Walizungumzia uwezekano wa kuitishwa hivi karibuni mkutano wa kimataifa wa wafadhili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW