1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Naibu mkuu wa idara ya Ujasusi ya Urusi apigwa risasi

6 Februari 2026

Naibu mkuu wa idara ya ujasusi wa kijeshi wa Urusi luteni jenerali Vladimir Alekseyev amepigwa risasi na kujeruhiwa mjini Moscow .

Urusi 2023 | Vladimir Alekseyev
Naibu mkuu wa idara ya ujasusi wa kijeshi wa Urusi luteni jenerali Vladimir Alekseyev akizungumza baada ya kusainiwa mkataba wa ushirikiano katika vita nchini Ukraine mnamo Juni 14, 2023Picha: Russian Defence Ministry/REUTERS

Katika taarifa, msemaji wa Kamati ya Uchunguzi Svetlana Petrenko, amesema Alekseyev alipigwa risasi mara kadhaa na washambuliaji wasiojulikana katika jengo moja la makazi kaskazini magharibi mwa moscow na baadaye kukimbizwa hospitalini.

Hata hivyo Petrenko hakutaja aliyehusika katika shambulizi hilo dhidi ya Alekseyev ambaye amehudumu kama naibu mkuu wa idara ya kijasusi ya Urusi tangu 2011.

Tukio hilo linakuja siku moja tu baada ya wajumbe wa Urusi, Ukraine na Marekani kumaliza mazungumzo ya siku mbili Abu Dhabi yaliyolenga kumaliza mzozo Ukraine ambao umedumu kwa takriban miaka minne.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW