Naibu Kamishna wa Polisi akamatwa kwa mashambulizi Ethiopia
25 Juni 2018Matangazo
Watu 30 wamekamatwa kuhusiana na mlipuko huo wakiwemo polisi kadhaa, akiwemo naibu kamishna wa polisi wa Addis Ababa.
Shambulizi hilo lilitokea katika uwanja mkubwa wa wazi uliokuwa umefurika, wakati Waziri Mkuu Abiy Ahmed akikamilisha hotuba yake mbele ya maelfu ya watu siku ya Jumamosi.
Vurugu zilizozuka baada ya mripuko huo wakati watu walianza kukimbilia jukwaani ziliwajeruhi watu 150.
Hakuna aliyetangaza kuhusika na shambulizi hilo lisilo la kawaida katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, ambao kila mara huwa na ulinzi mkali.
Ethiopia imesema kuwa Marekani itawatuma wapelelezi wa FBI ili kusaidia kuchunguza shambulizi hilo.