1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Naibu Rais wa Kenya 'anaumwa sana' mawakili wake wasema

17 Oktoba 2024

Wakili mkuu wa naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua aliambia baraza la seneti kuwa Gachagua "anaumwa sana" na amelazwa hospitali.

Kenya | Baraza la Seneti mjini Nairobi
Baraza la seneti nchini Kenya lajadili mashtaka ya kumuondoa naibu rais Rigathi Gachagua madarakani.Picha: Tony Karumba/AFP/Getty Images

Mawakili wanayemuwakilisha Naibu wa Rais nchini Kenya Rigathi Gachagua katika kesi ya kuondolewa kwake madarakani wameondoka katika bunge la seneti huku vikao vikiendelea baada ya bunge hilo kuamua kuendelea na vikao hivyo bila uwepo wa mteja wao, Gachagua.

Wakili mkuu wa naibu huyo wa rais alikuwa ameliambia bunge hilo kuwa Gachagua "anaumwa sana" na amelazwa hospitali.

Wakili Paul Muite amesema kwamba Gachagua ana maumivu makali ya kifua.

Hii ni baada ya Naibu huyo wa rais kushindwa kurudi katika bunge hilo kutoa ushahidi kama ilivyokuwa imeratibiwa.

Gachagua aliyekuwa bungeni katika kikao cha asubuhi alikuwa anatarajiwa kujitetea kwenye kikao cha mchana kuhusu madai 11 yaliyowasilishwa mbele ya Baraza la Seneti siku ya Alhamisi, kabla maseneta kupiga kura ya kumuondoa madarakani baadae Alhamisi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW