Timur Ivanov akamatwa kwa madai ya rushwa, Urusi
24 Aprili 2024Matangazo
Kukamatwa kwa ghafla kwa mshirika wa waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu, ambaye Putin alimpa jukumu la kupigana vita nchini Ukraine, kumeibua uvumi kuhusu vita dhidi ya ufisadi uliokithiri miongoni mwa viongozi wakuu wa jeshi na umma.
Waziri wa Ulinzi wa Ukraine kuondolewa katika wadhifa wake
Ikulu ya Kremlin imesema kwamba rais Putin amefahamishwa, kuhusu madai yanayomkabili Ivanov, ambaye amehudumu kama naibu waziri tangu 2016, chini ya majukumu yake alihusika pia na usimamizi wa majengo, makaazi, ujenzi na mikopo ya nyumba.
Iwapo atapatika na hatia, Ivanov anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela. Hata hivyo wizara ya ulinzi haikutoa tamko lolote.