1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI ; Askofu auawa

15 Julai 2005

Askofu wa kanisa katoliki Luigi Locati ameuawa nchini Kenya kwa kupigwa risasi ya kichwa katika dayosisi yake kaskazini mashariki mwa Kenya.Polisi ya Kenya inatuhumu , mauaji hayo yanahusiana na mapigano yaliyotokea kaskazini mwa nchi hiyo ambapo makasisi katoliki wanajaribu kuwasaidia watu.

Wakati huo huo habari zaidi zinasema ,wanakijiji katika sehemu hiyo wanakimbia makwao kutokana na mapigano .

Afisa mmoja wa chama cha msalaba mwekundu amesema kwamba wanakijiji wapatao alfu sita wameshakikimbia kijiji chao kufuatia mauaji halaiki ya watu 76.

Serikali ya Kenya imepeleka polisi zaidi katika sehemu hiyo iliyopo karibu na mpaka wa Ethiopia ambapo watu wa makabila ya Borana na Garba wanapigania maji na ardhi.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW