NAIROBI: Kenya kujengewa uwanja wa riadha
13 Januari 2004Matangazo
Waziri wa michezo wa Kenya, Najib BALALA ametangaza kuwa Qatar imekubali kuijengea Kenya uwanja wa michezo na riadha baada ya kutoa uraia kwa wanariadha wake 2, ambao sasa wanakimbia kwa jina la Qatar. Bwana BALALA aliyasema hayo baada ya kurejea kutokea Qatar akitaja kuwa uwanja huo utajengwa katika mji wa mashariki wa Eldoret. Waziri wa michezo wa Kenya anasema kuwa msaada huo umetolewa baada ya mazungumzo yake na kiongozi wa Qatar, Hamad Ben Khalifa al-THANI. Wanariadha hao waliopewa uraia wa Qatar ni Stephen CHERONO na Albert CHEPKIRUI. Bwana BALALA amesema Kenya haiwakatazi wanariadha wake kuchukua uraia wa kigeni isipokuwa inajifunza jinsi ya kuwalipa bora zaidi ili kuzuwia mtindo huo kushika kasi miaka ijayo.
