NAIROBI: Kenya kukosa msaada wa Canada
1 Aprili 2005Serikali ya Canada imeonya kwamba wafadhili kutoka nje wamepoteza tamaa ya kuisadia Kenya kufuatia kuongezeka kwa madai ya Ufisadi katika serikali ya rais Mwai Kibaki.
Madai ya ufisadi nchini Humo yamewahusisha zaidi viongozi wa serikali ambapo Canada inasema hilo limewarudisha nyuma sio tu Canada lakini hata wafadhili wengine.
Hata hivyo waziri wa fedha nchini Kenya David Mwiraria amelaumu madai hayo huku akiyataja kuwa ni hila iliyoipaka matope nchi yake.
Amesema tume ya kupambana na ufisadi nchini humo imependekeza kufunguliwa mashtaka juu ya njama 3 za ufisadi kati ya 20 zilizogunduliwa na Balozi wa Uingereza nchini Kenya Edward Clay zinazoihusiha moja kwa moja serikali ya kenya.
Marekani na Ujerumani tayari wamesimamisha msaada kwa Kenya huku Benki kuu ya dunia na Japan zikionya iwapo hatua hazitachukuliwa kumaliza Ufisadi.