1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Kenya kupata msaada wa fedha kutoka Ujerumani.

13 Mei 2005

Serikali ya Ujerumani imesema itatoa msaada wa fedha kiasi cha shilingi milioni mia tano kwa Kenya ambazo hapo awali zulizuiliwa kutokana na serikali ya Kenya kuwa legelege katika vita vya kupambana na rushwa.

Waziri wa sheria na masuala ya katiba nchini Kenya bwana Kiraitu Murungi amefahamisha hayo leo katika mahojiano na radio Deutsche Welle . Bwana Murungi anayefanya ziara ya siku sita hapa nchini Ujerumani, amesema kwamba wajumbe wa serikali ya Ujerumani wameridhika na juhudi zinazofanywa sasa na serikali ya Kenya katika kupambana na rushwa nchini.

Serikali ya Kenya imekuwa inalaumiwa sana ndani na nje ya nchi kutokana na tuhuma za kuwapo rushwa ya kiwango cha juu katika taasisi za serikali.

Waziri Murungi pia amefahamisha kwamba Kenya inatarajia kuwa na katiba mpya hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu baada ya wananchi kupiga kura.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW