Nairobi. Kenya yaanzisha uhusiano wa kibalozi na Sahara magharibi.
26 Juni 2005Kenya jana ilishtua juhudi zilizokwama za kidiplomasia za kutatua mzozo wa muda mrefu kati ya Morocco na Algeria juu ya Sahara magharibi, kwa kutambua rasmi uhuru wa jimbo hilo na kupambana na shutuma kali kutoka serikali ya Morocco.
Hatua hiyo inayopelekea kuleta mvutano ambayo imesababisha Morocco kumrejesha balozi wake kutoka Kenya ilifikiwa mjini Nairobi na wawakilishi wa chama cha Polisario ambacho kimekuwa kikipigana kudai uhuru katika nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini ya Phosphate, tangu pale koloni hilo la zamani la Hispania lilipochukuliwa na Morocco miaka 30 iliyopita.
Tumeamua kuanzisha uhusiano wa kibalozi na nchi hiyo, ikiwa ni mara ya kwanza msemaji wa serikali ya Kenya Alfred Mutua, kusema hivyo akiitaja nchi hiyo kuwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kiarabu ya Sahrawi.
Amesema kuwa jamhuri hiyo iko huru sasa kufungua ubalozi wake ama mwakilishi wa kidiplomasia nchini Kenya , lakini hii haimaanishi kuwa Kenya inaweza kufungua nayo ubalozi wake nchini humo, kwa kuwa amesema Sahara magharibi bado inadaiwa kuwa sehemu ya Morocco na inatawaliwa na taifa hilo.