1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Kenya yachangia majeshi.

19 Mei 2005

Waziri wa usalama wa taifa nchini Kenya bwana John Muchuki amesema kwamba nchi yake itapeleka askari 842 kuchangia katika jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani kusini mwa Sudan ili kusaidia katika utekelezaji wa mapatano ya kumaliza vita ya zaidi ya miaka ishirini nchini Sudan.

Bwana Muchuki amesema hayo leo mjini Nairobi kwenye mkutano na mkuu wa majeshi ya Sudan jenerali Arabi Abdullah Ahmed .mjini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha idadi ya askari alfu 10 watakaosimamia utekelezaji wa mapatano ya kumaliza vita baina ya majeshi ya serikali ya Sudan na waasi wa kusini yaliyofikiwa mapema mwezi januari.

.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW