NAIROBI : Kiongozi mtuhumiwa wa Mungiki mbaroni
24 Agosti 2007Matangazo
Polisi ya Kenya imemkamata kiongozi mtuhumiwa wa kundi lililopigwa marafuku la Mungiki linalolaumiwa kwa matukio kadhaa ya kuchinja watu katika miezi ya hivi karibuni.
Eric Kiraithe msemaji wa polisi amesema Njoroge Kamunya ambaye amekuwa mitini kwa miaka miwili alikamatwa hapo Jumanne katika viunga vya mji mkuu wa Nairobi.
Amesema polisi inamchunguza kuhusiana na wizi wa kutumia nguvu.
Kamunya ni kaka wa Maina Njenga kiongozi wa zamani wa kundi la Mungiki ambaye hapo mwezi wa Juni alihukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani kwa kumiliki silaha kinyume na sheria.