1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Maharamia waiacha meli huru.

3 Oktoba 2005

Maharamia wa Kisomalia ambao waliteka nyara meli iliyokodishwa na umoja wa mataifa ikichukua shehena ya chakula cha msaada kwa ajili ya wahanga wa maafa ya tsunami zaidi ya miezi mitatu iliyopita wameitelekeza meli hiyo jana Jumapili na kuruhusu wafanyakazi wa meli hiyo kuwa huru.

Maafisa waliohusika katika sakata hilo, wamesema kuwa watu hao wenye silaha , ambao waliiteka nyara meli hiyo MV Semlow hapo Juni 27 na kukataa madai ya mpango wa chakula wa umoja wa mataifa WFP, wa kuiachia meli hiyo bila masharti , waliondoka katika meli hiyo jana Jumapili mchana wakati ikivutwa na meli nyingine iliyotekwa nyara.

Karim Kudrathi , mkurugenzi wa kampuni ya wakala wa meli ya Motaku yenye makao yake makuu mjini Mombasa ambao ni wamiliki wa meli hiyo , amesema kuwa baada ya mfanyabiashara mmoja wa Kisomali kuingilia kati wateka nyara hao wakaamua kuiachia huru.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW