Nairobi. Maharamia washambulia watalii.
6 Novemba 2005Matangazo
Meli ya kitalii iliyochukua zaidi ya abiria 300 imenusurika shambulio la maharamia nje ya pwani ya Somalia. Msemaji wa kampuni ambayo inaendesha meli hiyo amesema kuwa watu wenye silaha wakiwa katika boti yendayo mbio waliikaribia meli hiyo kiasi cha kilometa 160 kutoka katika pwani ya Somalia .
Watu hao walifyatua risasi pamoja na makombora dhidi ya meli hiyo katika juhudi za kutaka isimame ili waingie katika meli hiyo.
Nahodha wa meli hiyo alibadilisha mwelekeo na kuongeza kasi ndipo wakafanikiwa kuwakimbia maharamia hao.
Mfanyakazi mmoja katika meli hiyo imejeruhiwa kidogo katika tukio hilo.
Wasafiri katika meli hiyo ni watu waliokuwa wakifurahia likizo zao kutoka bara la Ulaya na Marekani.