1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Maombi ya wakimbizi wa kisiasa yamiminika

25 Juni 2005

Waomba hifadhi ya kisiasa nchini Kenya,kwa maelfu wamepeleka maombi yao ya kutaka vyeti vya ukimbizi,siku chache tu kabla ya kumalizika ule muda wa kujiandikisha au kukabiliwa na kitisho cha kurejeshwa makwao kwenye vita na njaa.Kenya ina kiasi ya wakimbizi 250,000 waliokimbia migogoro katika nchi za jirani za Sudan,Somali na Ethiopia.Lakini wachambuzi wanasema,wengine kwa maelfu wamejipenyeza mipakani na wanaishi Kenya kinyume na sheria.Kwa mujibu wa Emmanuel Nyabera,msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNHCR linaloshughulikia wakimbizi duniani,tatizo kubwa ni kutambua nani alie mkimbizi halisi na nani aliehamia Kenya kinyume na sheria.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW