1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Mbabe wa vita airudisha ofisi ya Umoja wa Mataifa

13 Septemba 2005

Mkuu wa wanamgambo ambaye alikuwa mwenyeji wa serikali dhaifu ya Somalia ameirudisha kwenye udhibiti wa Umoja wa Mataifa ofisi ya masuala ya msaada wa kibinaadamu ambayo aliinyakuwa siku mbili zilizopita katika mji mkuu wa kujishikiza wa Jowhar nchini Somalia.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema mbabe huyo wa vita Mohammed Omar Habeeb alizirudisha funguo za ofisi hiyo kwa Shirika la Kuwahudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF mapema leo hii.

Habeeb ambaye anajulikana zaidi kwa jina la utani la Mohamed Dheere hakutowa maelezo yoyote ya kuinyakuwa ofisi hiyo hatua ambayo imetibuwa shuhuli za misaada ya kibinaadamu.

Mipango ya shughuli za UNICEF katika mji wa Jowhar inajumuisha maji,elimu,UKIMWI na virusi vya HIV pamoja na miradi ya vijana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW