Nairobi. Mkutano kuangalia sera za biashara ya kimataifa.
14 Septemba 2005Matangazo
Mkutano wa maendeleo ya biashara katika bara la Afrika unaodhaminiwa na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP , umeanza rasmi mjini Nairobi leo.
Mkutano huo utakaofanyika kwa muda wa siku tatu unahudhuriwa na zaidi ya mataifa 22 ya Afrika.
Mawaziri wa biashara na wawakilishi kutoka mashirika ya biashara barani Afrika wanazungumzia juu ya sera za biashara ya kimataifa na jinsi wawekezaji kutoka nchi za nje wanavyoathiri biashara na uchumi wa bara hilo.