1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Moi apinga rasimu ya katiba mpya

28 Agosti 2005

Rais mstaafu wa Kenya Daniel arap Moi ambaye karibu muongo mmoja uliopita alianzisha mchakato wa kuchambuwa mpya sheria ya msingi ya nchi hiyo iliokuwepo tokea wakati wa uhuru leo hii ameibeza rasimu ya katiba mpya kwa kusema inaleta uhasama,tuhuma na kutoaminiana miongoni mwa wananchi.

Rasimu hiyo ambayo ilichapishwa wiki iliopita inaendelea kushikilia madaraka kamili kwa Rais,inaruhusu mahkama za kidini hasa zile za Kiislam na kuweka uwezekano wa kutungwa sheria yenye kuruhusu utowaji wa mimba pamoja na madai ya kuwa ina mianya ya kuruhusu ndoa za mashoga.

Moi amesema katika taarifa kwamba hawezi kuunga mkono waraka wenye kuleta uhasama,tuhuma na kutoamininiana miongoni mwa wananchi.

Wakati karibu wananchi wote walikuwa wakitaka madaraka ya sasa ya Rais yapunguzwe watu wachache wenye ushawishi mkubwa serikalini wameweza kurekebisha rasimu hiyo kwa kuendelea kushikilia madaraka hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW