NAIROBI: Mpigania uhuru afariki.
9 Machi 2005Matangazo
Kiongozi muhimu katika mapambano nchini Kenya ya kudai uhuru, Bwana Bildad Kagia, amefariki dunia baada ya maisha yake ambayo yaliambatana na mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni wa Uingereza na baadaye hali ya ufukara na tena kutengwa chini ya utawala ulioingia madarakani wakati wa uhuru.
Bintiyake Njoki Kaggia ameliambia shirika la habari la reuters, kiongozi huyo wa chama cha wafanyakazi, ambaye anafahamika sana kwa upingaji wake mkubwa wa viongozi wapenda madaraka na ufisadi, alifariki siku ya Jumatatu baada ya kupata kiharusi akiwa na umri wa miaka 84.