1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Mvua kubwa zimesababisha mafuriko Afrika Mashariki

4 Desemba 2006

Mafuriko mabaya kabisa kupata kutokea tangu miaka kadhaa,yameuwa hadi watu 150 katika nchi za Afrika ya Mashariki.Mamilioni ya watu pia wamepoteza makazi yao.Wafanyakazi wa mashirika yanayotoa misaada wanasema Somalia,Ethiopia,Kenya na Rwanda zimeathirika vibaya kwa mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha mafuriko majuma ya hivi karibuni.Ripoti zinasema,zaidi ya watu 100 wamepoteza maisha yao nchini Somalia peke yake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW