Nairobi. Naibu mkuu wa kundi la LRA hajuliani aliko.
7 Novemba 2007Matangazo
Naibu mkuu wa kundi la waasi wa Lord’s Resistance Army hajulikani aliko baada ya kutokea tofauti ndani ya kundi hilo kuhusiana na mazungumzo ya amani yanayolegalega na serikali. Magazeti nchini Uganda yamedai kuwa Vincent Otii ameuwawa mwezi uliopita, licha ya afisa wa LRA kuliambia shirika la habari la AFP kuwa madai hayo ni upuuzi mtupu, na kusisitiza kuwa yu hai.
Afisa mmoja wa kundi la Sudan Peoples Liberation Movement ambalo linamahusiano na viongozi wa LRA ameliambia shirika la habari la AFP kuwa kulitokea mapigano miongoni mwa kundi la LRA kundi moja linalomuunga mkono kiongozi wa waasi Joseph Kony likitaka kuachana na mapambano ya silaha na kutoka msituni wakati kundi la Otti likitaka kuendelea kupambana na serikali.