NAIROBI: Obama awasili Kenya
24 Agosti 2006Matangazo
Barack Obama, mmarekani pekee mwenye asili ya kiafrika katika baraza la senate nchini Marekani, amewasili nchini Kenya leo jioni, nyumbani kwa baba yake marehemu, mkulima mfugaji aliyesomea katika chuo kikuu cha Havard na kuhitimu kama mwanauchumi.
Obama atapimwa ukimwi hadharani katika zahanati ndogo mjini Nyangoma Kogelo, alikokulia babake na ambako mpaka sasa bibi yake anaishi.
Obama atakutana na rais Mwai Kibaki wa Kenya, na maofisa wa wizara ya mambo ya kigeni kabla kutembelea eneo la shambulio la bomu la mwaka wa 1998 mjini Nairobi, ambapo watu 248 waliuwawa.
Baadaye ataendelea na ziara yake nchini Djibouti na Chad.