1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Ofisi za umoja wa mataifa zavamiwa Somalia.

13 Septemba 2005

Kiongozi mmoja wa wapiganaji wa kiukoo kusini mwa Somalia amevamia ofisi za umoja wa mataifa katika mji ambao serikali ya muda ya nchi hiyo ina makao yake makuu.

Afisa mwandamizi wa umoja wa mataifa amesema jana kuwa kiongozi wa jimbo la kusini kati nchini Somalia la Shabelle, Mohammed Dheere, aliingia katika ofisi za shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia watoto siku ya Jumapili katika mji wa Jowhar, kilometa 90 kaskazini mashariki ya mji mkuu Mogadishu na kuwaambia wafanyakazi kumpatia funguo, amesema Christian Balslev-Olesen , mkuu wa shirika hilo nchini Somalia , ambayo ina makao yake makuu katika nchi jirani ya Kenya kwa kuwa taifa hilo la pembe ya Afrika halina usalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW