1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Rais wa Somalia aahidi kutotumia nguvu kusalimisha silaha za wanamgambo

21 Agosti 2005

Rais wa Somalia ameahidi leo hii kutumia ushawishi badala ya nguvu kusalimisha silaha za wanamgambo wake wengi kwa kusema kwamba wababe wa vita na wafanya biashara wanapaswa kungamuwa kwamba ni kwa faida yao wenyewe kusalimisha silaha za wanamgambo wanaowadhibiti.

Katika mahojiano na shirika la habari la Uingereza Reuters Rais Abdulahi Yusuf ambaye serikali yake imekumbwa na mabishano juu ya mahala inapopasa kuweka makao yake makuu ameongeza kusema kwamba ana imani kuwa iko siku ataweka serikali yake hiyo mjini Mogadishu lakini amesisitiza kwamba kwa sasa mji huo mkuu bado ni wa hatari.

Akiwa nchini Kenya kuelekea Saudi Arabia kujadili uwezekano wa kupatiwa msaada kwa serikali yake Yusuf amesema wataleta utulivu nchini kote Somali kwa kupitia maridhiano kwa kushawishiana na kuleta usuluhishi wa makabila yaliyokuwa yakipigana wakati wa vita nchini humo.

Lakini amesema katu hawatoleta utulivu nchini Somalia kwa kwa kutumia nguvu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW