1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Rais wa zamani wa Marekani aahidi kuisaidia Kenya kupambana na ukimwi.

23 Julai 2005

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton jana aliahidi kuisaidia Kenya kupambana na ugonjwa wa ukimwi, hususan katika kutoa huduma ya afya bure kwa watoto katika maeneo ya vijijini.

Clinton amesema kuwa shirika lake la kutoa misaada hadi sasa limepokea dola milioni 1.5, ili kusaidia kuwapa mafunzo wafanyakazi wa utibabu na kuwapeleka huko vijijini nchini Kenya, ambako ukimwi umesababisha kiasi cha watu milioni 1.5 kufariki tangu mwaka 1984.

Katika kiasi cha watu 200,000 ambao wanahitaji haraka dawa za kurefusha maisha nchini Kenya, ni watu 40,000 tu ambao wanapata dawa hizo.

Wakati huo huo rais huyo wa zamani wa Marekani jana aliwataka Wakenya wenye hasira kuchukua hatua za amani chini ya mfumo wa kidemokrasia , baada ya mtu mmoja kuuwawa katika maandamano yaliyoambatana na ghasia dhidi ya mageuzi ya katiba ambayo yatampa madaraka zaidi rais wa nchi hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW