1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Repoti ya bunge yamhusisha Biwott na kifo Cha Ouko

14 Mei 2005

Nicholas Biwott mwanasiasa mwandamizi wa upinzani nchini Kenya hapo jana ameshutumu kuwa ni upuuzi repoti ya bunge ambayo imependekeza achunguzwe kuwa uwezekano wa kuhusika na mauaji ya waziri wa mambo ya nje hapo mwaka 1990.

Kitendawili kuhusiana na kifo cha Waziri wa mambo ya nje Robert Ouko ambaye mwili wake uliokatwa katwa ulikutikana na wachungaji kwenye mlima karibu na nyumbani kwake kinaendelea kuwaandama Wakenya wenye shaku ya kutendeka haki katika nchi hiyo iliochafuliwa jina na historia ya mauaji ya kisiasa.

Biwott ambaye wakati fulani alikuwa mshirika wa karibu wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Daniel rap Moi siku zote amekuwa akikanusha kuhusika na mauaji hayo na ameshinda kesi mbali mbali za kuchafuliwa jina dhidi ya magazeti ambayo yamedokeza kuhusika kwake katika kifo cha Ouko.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW