1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Rwanda kushambulia waasi Congo.

6 Septemba 2005

Waasi wa Kihutu nchini Rwanda wanaofanya shughuli zao katika eneo la mashariki ya jamhuri ya kidemokrasi ya Congo DRC, wameishutumu serikali ya Rwanda kwa kupanga njama za kushambulia eneo hilo la Congo.

Katika taarifa iliyopatikana na shirika la habari la AFP leo, majeshi ya kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda FDLR, imesema kuwa Rwanda inajitayarisha kufanya shambulio kubwa kabisa kuwahi kufanyika katika eneo hilo.

Kundi hilo la FDLR, limesema kuwa serikali ya Rwanda imeweka kikosi cha wapiganaji katika eneo la Kivuye, Nyange na Kinyana katika jimbo la kaskazini la Kivu nchini Congo na kwamba vikosi hivyo vinasubiri amri kutoka Kigali ili kuanza mashambulizi hayo.

Rwanda imekuwa ikiwashutumu wapiganaji hao, ambao wamekuwa wakijificha katika misitu mashariki ya Congo kwa muda wa miaka 11 sasa, kwa kuhusika katika mauaji ya halaiki nchini humo mwaka 1994, ambapo watu zaidi ya 800,000 wameuwawa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW