1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Schroeder azuru Kenya baada ya Ethiopia

20 Januari 2004

Kansela Gerhard SCHROEDER aliwasili jana jioni katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi akitokea Addis Ababa, Ethiopia, ambako ameahidi kuwa Ujerumani itasaidia Afrika kudumisha amani na kupambana na umaskini. Baada ya Kenya, Bwana SCHROEDER atazuru Afrika ya Kusini na Ghana katika duru ya kwanza rasmi ya Kansela wa Ujerumani barani Afrika. Kwa mujibu wa taarifa za wizara ya ushirikiano mjini Berlin, Bwana SCHROEDER anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo baadaye leo na mwenyeji wake Rais Mwai KIBAKI na kumthibitishia hatua ya Ujerumani ya kuizidishia Kenya msaada wake wa maendeleo. Duru hizo zimetaja pia kuwa Ujerumani inakusudia kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi wa Kenya pamoja na kuzidisha ushirikiano wa idara za upelelezi hasa katika mapambano dhidi ya ugaidi. Alipokuwa mjini Addis Ababa na kuhutubia maafisa wa Muungano wa Afrika, Bwana SCHROEDER alitangaza msaada wa Euro laki 6,5 za kuchangia harakati za Umoja huo za kulinda amani Liberia, Sudan, Somalia na Burundi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW