1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi. Wakimbizi wakosa chakula kusini mwa Sudan.

27 Agosti 2005

Umoja wa mataifa umesema jana kuwa unapata taabu kuweza kuwalisha wakimbizi 90,000 wa Eritrea na Ethiopia walioko mashariki ya Sudan , kukiwa na asilimia 50 ya ukosefu wa fedha na chakula.

Mkurugenzi wa shirika la mpango wa chakula la umoja wa mataifa nchini Sudan Ramiro Lopes da Silva amesema kuwa shirika hilo linahitaji msaada wa kimataifa ili kuendelea kuwalisha wakimbizi hao , kwa kuwa hali yao ni mbaya sana.

Wakimbizi walianza kuingia nchini Sudan katika miaka ya 1970 na 80 wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe, ukame na njaa nchini Ethiopia vilipowalamisha maelfu kuikimbia nchi hiyo.

Idadi ya wakimbizi iliongezeka zaidi baada ya vita vya mpaka kati ya Eritrea na Ethiopia katika miaka ya 1990.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW