NAIROBI: Wasomali zaidi wanahitaji misaada ya kiutu
25 Agosti 2007Matangazo
Idadi ya watu wanaohitaji misaada ya kiutu nchini Somalia,imeongezeka kwa asilimia 50 na kufikia milioni moja na nusu.Kwa mujibu wa kundi linalogharimiwa na wafadhila-FSAU,maeneo yaliyokuwa yakitoa chakula,yamepata mavuno mabaya.Mvua pia zimeharibu miundo mbinu ya umwagiliaji maji mashambani,katika nchi hiyo iliyokumbwa na migogoro.
Idadi ya watu wanaohitaji misaada imeongezeka sana tangu zilipomalizika mvua zilizonyesha kati ya Oktoba na Desemba nchini Somalia.