NAIROBI
25 Mei 2005Matangazo
Jaji wa mahakama kuu mjini Nairobi Kenya, Aggrey Muchelule amefutilia mbali pendekezo la mawakili wa watuhumiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi la kundi la al-Qaeda katika hoteli moja ya watalii mjini Mombasa mwaka wa 2002, la kutaka mashtaka yote yafutwe.
Muchelule amesema kila mmoja wa watuhumiwa hao ana kesi ya kujibu, kwa kuhusika katika kupanga shambulio la bomu dhidi ya hoteli ya Paradise na njama ya kuitengua ndege ya Israel wakati ilipokuwa ikiondoka kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mombasa.
Watu 18 waliuwawa katika shambulio hilo la bomu wakiwemo watu watatu wa kujitoa muhanga.