NAIROBI
15 Februari 2005Matangazo
Waziri Mkuu wa serikali ya mpito yaq Somalia,Mohammed Ali Gedi amesema kuwa serikali yake ambayo inafanya kazi zake ikiwa uhamishoni mjini Nairobi,huenda isiwe katika nafasi nzuri ya kufikia lengo lililowekwa la tarehe wiki ijayo ya kuanza kujizatiti ndani ya nchi ya Somalia.
Bwana Gedi ambaye wiki iliyopita alisema serikali yake itaanza kuondoka mjini Nairobi kuelekea katika mji mkuu wa Somalia,Mogadishu kuanzia tarehe 21 mwezi huu,amesema serikali yake kwanza inasubiri kusikia kutoka kwa wajumbe watatu zaidi walio katika baraza la mawaziri la nchi hiyo wanaotathmini hali halisi ya usalama huko Somalia.
Wajumbe hao wanatazamiwa kuelekea Somalia kesho lakini hawatoweza kuandaa ripoti kamili hadi baadae mwezi huu.