1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Chama cha ODM-K chateu mgomea wake wa urais

31 Agosti 2007

Chama cha Orange Democratic Movement Kenya-ODM K kinafanya mkutano wa kuteua mgombea wake wa urais katika uchaguzi unaopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Yapata wanachama 4200 wanakutana mjini Nairobi kuchagua kati ya Mbunge wa Mwingi kaskazini Kalonzo Musyoka na Dr Julia Ojiambo kiongozi wa chama cha leba cha LPK.

Mgombea wa chama cha ODM-K atakuwa mmoja wa wagombea wa urais akiwemo pia rais aliyeko madarakani Mwai Kibaki pamoja na mwakilishi wa chama cgha ODM atakayechaguliwa hapo kesho.

Chama cha ODM kilivunjika vipande viwili katikati ya mwezi huu huku Kalonzo Musyoka akijiondoa na kuongoza ODM-K na Raila Odinga na vigogo wengine kusalia na ODM asili.

Mapema wiki hii rais mstaafu Daniel arap Moi alitangaza kuwa anamuunga mkono Rais Mwai Kibaki kurejea tena madarakani kwa muhula wa pili na wa mwisho.Tarehe hasa ya Uchaguzi wa serikali za mitaa,wabunge na rais bado haijatangazwa.Hii ni mara ya nne kwa uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi kufanyika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW