1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI:Vikosi vya Ethiopia ndani ya Somalia.

21 Julai 2006

Vikosi vya Ki-Ethiopia nchini Somalia huenda vikaipa serikali ya mpito ya Somalia uwezo pekee wa kupigana na kuwazuia wanamgambo wa Kiislamu kudhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo kwenye Pembe ya Afrika.

Lakini hicho pia kinaweza kuwa kisingizio kinachohitajiwa na wanamgambo hao ili umma upate kuwaunga mkono katika vita vya kigaidi.Wakaazi wa Baidoa,waliripoti kuwa waliona vikosi vya Ki-Ethiopia vikiwasili katika mji huo katika magari ya kijeshi yaliyopakiwa zana.

Siku ya Jumatano wanamgambo wa Kiislamu walijongelea mji wa Baidoa ulio makao ya serikali ya mpito.Maafisa wa Ethiopia wamekanusha kuwa majeshi yao yameingia Somalia.

Lakini siku moja kabla ya hapo,waziri wa habari wa Ethiopia aliapa kuwa wanamgambo hao wa kiislamu watatimuliwa ikiwa watajaribu kuudhibiti mji wa Baidoa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW