1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi.Waasi wa kusini mwa Sudan wanataka Marekani kuondoa vikwazo vya biashara nchini Sudan.

14 Mei 2005

Waasi wa zamani wa kusini mwa Sudan wamesema jana kuwa wamekuwa na mazungumzo na serikali ya Marekani kuhusiana na kuondolewa katika eneo hilo vikwazo vilivyowekwa mwaka 1997 dhidi ya nchi hiyo.

Chama cha waasi wa Sudan Peoples Liberation Army SPLA kilitia saini makubaliano ya amani na serikali ya Sudan Januari mwaka huu makubaliano yaliyomaliza vita vilivyodumu zaidi ya miongo miwili kusini mwa nchi hiyo.

Makamu mwenyekiti wa chama cha SPLA Riek Machar amewaambia wawekezaji katika mkutano mjini Nairobi kuwa wasikatishwe tamaa na vikwazo hivyo vya Marekani.

Bwana Machar amesema kuwa vikwazo hivyo ambavyo vimezuwia masuala ya kibiashara na kuzuwia makampuni yenye makao yake nchini Marekani kuweka vitega uchumi nchini Sudan , vinakwamisha utekelezwaji wa makubaliano ya amani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW