1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nairobi.Wamasai nchini Kenya wadai mabadiliko ya hali ya hewa yanaharibi masingira yao asili.

10 Novemba 2006

Wanachama wa jamii ya Wamasai nchini Kenya hii leowametoa mwito kutaka hatua za dharura zichukuliwe kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, wakisema kuwa, hali ya ujoto duniani ambao wao sio sababu, inaharibu hali yao ya maisha ya kijadi.

Wakizungumza pembezoni mwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa unaofanyika katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, wanachama hao wamesema maeneo yao ya kilimo yanatishiwa na ongezeko la gesi kutoka katika nchi zinazoendelea.

Akizungumzia khofu yao inayowakabili, mwanamama wa kimasai Sharon Looremetta amesema, jamii ya kimasai wanahisi na kushtushwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Looremetta ameongeza kuwa kwa kipindi cha misks mitatu wamepata mvua chache tu jambo ambalo linawapa wasi wais mkubwa juu ya mabadiliko hayo ya hali ya hewa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW